Qur'an ni nini?
👉 Ni muujiza wake wa mwisho, (muujiza, "tunamaanisha kufanyika jambo lisilo la kawaida au la ajabu, jambo ambalo haliwezi kufanywa na wanadamu kikawaida).
Qur'an ndiyo maneno ya mwisho ya Mwenyezi Mungu
👉 Yalifunuliwa kwa Nabii Muhammad (iwe juu yake amani) na Malaika Gabriel (Jibril).
Qur'an ni kitabu kinachoelezea utukufu wa Mwenyezi Mungu na maajabu ya uumbaji wake. Pia huonyesha rehema za Mwenyezi Mungu na haki, hutoa majibu ya siri za maisha kama vile;
Wapi nilitoka, kipi kitakachotokea baada ya kifo, kusudio la kuumbwa ..Inatoa muongozo kwa kila nyanja ya maisha ya mwanadamu, kutoka kwenye uchumi na maadili ya biashara hadi kwenye ndoa.
Qur'an sio tu ya kipekee katika njia ambayo inatoa mada zake, lakini pia ni ya kipekee kwa kuwa yenyewe ni muujiza.
👉 Qur'an imeepukana na makosa yote au utata wowote, licha ya kuwa ilifunuliwa kwa kipindi cha miaka 23.
Watu wa sasa hushangazwa na namna Qur'an inaelezea ishara za uwepo wa Mwenyezi Mungu katika ulimwengu na jinsi kila kitu kwenye ulinwengu kilivyopangwa kwa uangalifu.
Ina maelezo ya kisayansi mengi ya kweli, kama vile kuhusu ukuaji wa mtoto tumboni ambayo imeelezwa kwa kina, jambo linalo washangazwa wanasayansi wengi kwa vipi maelezo kama haya yametajwa miaka 1400 iliyopita.
Je! Unakubaliana nami?